Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 20:27

Migogoro inayoendelea na watu kuhama makazi inasababisha njaa duniani; Guterres


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. March 1, 2023.

Zaidi ya asilimia 40 ya watu wanaohitaji chakula wanaishi huko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Afghanistan, Nigeria na Yemen, ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema

Takriban watu milioni 258 walihitaji misaada ya dharura ya chakula mwaka jana kwa sababu ya migogoro, matatizo ya kiuchumi na majanga ya hali ya hewa ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema Jumatano, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka milioni 193 mwaka uliopita.

"Zaidi ya robo ya watu bilioni moja hivi sasa wanakabiliwa na viwango vya juu vya njaa, na wengine wako kwenye ukingo wa kukumbwa na njaa. Hilo haliwezekani", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema. "Ilikuwa mbaya sana ya kutisha ya kushindwa kwa ubinadamu kufanya maendeleo. kumaliza njaa, na kufikia usalama wa chakula pamoja na kuboresha lishe kwa wote", alisema.

Zaidi ya asilimia 40 ya watu wanaohitaji chakula wanaishi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Afghanistan, Nigeria na Yemen, ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema.

Migogoro na watu wengi kuhama makazi yao kunaendelea kusababisha njaa duniani, alisema Guterres. Ongezeko la umaskini, kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, maendeleo duni, mgogoro wa hali ya hewa na majanga ya asili pia yanachangia ukosefu wa usalama wa chakula.

Mwaka 2022 watu milioni 258 walikabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama wa chakula katika nchi 58 au maeneo, kutoka milioni 193 katika nchi 53 mwaka uliopita, ripoti hiyo ilisema. Idadi hii sasa imeongezeka kwa mwaka wa nne mfululizo.

XS
SM
MD
LG