Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 09:07

Kijana ameokolewa akiwa hai baada ya saa 260 za tetemeko la ardhi huko Uturuki


Waokoaji Uturuki wakiendelea na shughuli za uokozi kufuatia tetemeko la ardhi la Februari 6
Waokoaji Uturuki wakiendelea na shughuli za uokozi kufuatia tetemeko la ardhi la Februari 6

Waokoaji wa Uturuki walifanikiwa kumtoa kijana mdogo akiwa hai kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka saa 260 baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rikta lililotokea kusini mashariki mwa Uturuki na Syria shirika la habari la serikali ya Uturuki Anadolu limeripoti Ijumaa.

Osman Halebiye mwenye umri wa miaka kumi na minne alipelekwa katika hospitali huko Antakya. Baadae wanaume wawili Mehmet Ali Sakiroglu mwenye miaka 26, na Mustafa Avci mwenye miaka 33 waliokolewa kutoka vifusi vya jengo hilo-hilo, shirika la habari DHA lilisema.

Baada ya kuokolewa, Avci alimuona mtoto wake mchanga kwa njia ya simu ya mkononi akiwa na wazazi wake kulingana na Reuters. Zaidi ya watu 41,000 nchini Uturuki na Syria wameuawa katika tetemeko la ardhi na maelfu wamekoseshwa makazi.

XS
SM
MD
LG