Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 15:47

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akutana na viongozi Tigray


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipokuwa Jimma Ethiopia, June 16, 2021.REUTERS
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alipokuwa Jimma Ethiopia, June 16, 2021.REUTERS

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alikutana na viongozi wakuu wa vikosi vya mkoa wa  Tigray siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza tangu watie saini mkataba wa amani na serikali ya kitaifa kumaliza miaka miwili ya vita, shirika la utangazaji la serikali lilisema.

Waziri Mkuu Abiy na maafisa wengine walikutana leo na kufanya majadiliano na ujumbe wa TPLF kuhusu maendeleo ya mchakato wa amani, Shirika la Utangazaji la Ethiopia lilisema kwenye akaunti yake ya Twitter.

Matokeo yake , Waziri Mkuu Abiy alipitisha maamuzi kuhusu kuongeza safari za ndege, benki na masuala mengine ambayo yangeongeza uaminifu na kurahisisha maisha ya raia.

Serikali ya Addis Ababa na vikosi vya chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) vilitia saini makubaliano mwezi Novemba kusitisha mapigano kabisa, na kumaliza mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu na mamilioni wengine kupoteza makazi yao.

Mkutano wa Ijumaa ulikuwa wa kwanza wa Abiy na wasimamizi wakuu wa eneo la kaskazini la Tigray tangu mapigano yazuke.

XS
SM
MD
LG