Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:25

Watoto wawili wamekufa na wengine kujeruhiwa baada ya kukanyaga guruneti


Mfano wa watoto waliokuwa wakicheza huko DRC na kukanyaga guruneti
Mfano wa watoto waliokuwa wakicheza huko DRC na kukanyaga guruneti

Kundi la vijana kadhaa lilikuwa linawinda ndege siku ya jumatatu  katika shamba lililo karibu na Ndunda kwenye eneo la Ruzizi katika jimbo la Kivu Kusini huko DRC ndipo walipojikwaa na kukanyaga guruneti

Watoto wawili wamefariki na watu sita wamejeruhiwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) baada ya guruneti waliloligundua wakati wanawinda ndege kulipuka maafisa wa eneo hilo walisema Jumanne.

Kundi la vijana kadhaa siku ya Jumatatu lilikuwa linawinda ndege katika shamba lililo karibu na Ndunda kwenye eneo la Ruzizi katika jimbo la Kivu Kusini ndipo walipojikwaa na kukanyaga guruneti.

"Watoto hawa walikichukua kifaa ambacho walidhani ni kitu cha kuchezea, bila kujua kwamba lilikuwa guruneti, na kisha li-lilipuka," alisema Gerard Matibu Mupanzi afisa wa eneo hilo.

Aliongeza kuwa msichana mmoja mwenye umri wa miaka mitatu alifariki katika mlipuko huo Jumatatu mchana, huku mvulana wa miaka 11 akifariki siku iliyofuata kutokana na majeraha aliyoyapata.

Watu wengine sita, wakiwemo watoto watatu, walijeruhiwa katika ajali hiyo.

Luteni Marc Elongo msemaji wa jeshi la Congo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba timu ya jeshi imekwenda huko Ndunda kuchunguza tukio hilo.

Zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanazunguka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mengi ni urithi wa vita vya kikanda vilivyozuka katika zama za karne.

XS
SM
MD
LG