Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:02

Ndege zizisizo na rubani za Korea kaskazini zimeingia katika anga ya Korea kusini


Mfano wa ndege zinazoshukiwa zisizotumia rubani zinaangaliwa kwenye wizara ya ulinzi mjini Seoul huko Korea Kusini, June 21, 2017. (Lee Jung-hoon/Yonhap via AP, File)
Mfano wa ndege zinazoshukiwa zisizotumia rubani zinaangaliwa kwenye wizara ya ulinzi mjini Seoul huko Korea Kusini, June 21, 2017. (Lee Jung-hoon/Yonhap via AP, File)

Ndege kadhaa zinazoshukiwa zisizokuwa na rubani (drones) za Korea Kaskazini ziliingia katika anga ya Korea Kusini siku ya Jumatatu kulingana na jeshi la Korea Kusini ambalo lilijibu kwa ndege za kivita na helikopta za mashambulizi.

Jeshi la Korea Kusini limesema limefyatua risasi za onyo na kujaribu kuangusha angalau moja ya drone hizo lakini likaelezea hali hiyo kuwa inaendelea saa sita na nusu baada ya kuanza.

Ndege ya kwanza isiyo na rubani ilivuka mstari wa kijeshi (MDL) katika eneo la mpaka wa jimbo la Gyeonggi saa 4:25 asubuhi kwa saa za Huko na kufuatiwa na nyingine kadhaa kulingana na maafisa wa jeshi la Korea Kusini.

Idadi kamili ya ndege zisizo na rubani haijulikani lakini ziko chini ya kumi, maafisa waliongeza.

XS
SM
MD
LG