Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:44

Russia inasema hakuna dalili za utayari wa amani kwa Ukraine


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiyy
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiyy

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba ziara ya Zelenskyy mjini Washington inaonyesha Marekani inapigana vita hivyo dhidi ya Russia lakini si moja kwa moja

Russia imesema alhamisi hakuna dalili za utayari kwa amani kutoka katika ziara ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy mjini Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden alimkaribisha Zelenskyy kwa mazungumzo huko White House na baadaye kiongozi huyo wa Ukraine alihutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani, ambapo alisema Ukraine "kamwe haitasalimu amri" katika vita vyake dhidi ya uvamizi ambao Russia ilivianzisha miezi 10 iliyopita.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba ziara ya Zelenskyy inaonyesha Marekani inapigana vita hivyo dhidi ya Russia lakini si moja kwa moja.

Marekani imetoa msaada mkubwa wa kijeshi na kibinadamu kwa Ukraine, na jumatano ilitangaza msaada mpya unaojumuisha makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot. Zelenskyy amesema mfumo wa hali ya juu zaidi utaisaidia Ukraine kukabiliana na mashambulizi ya makombora ya Russia ambayo yameikumba miji kadhaa nchini kwake na miundombinu muhimu.

Peskov amesema makombora ya Patriot hayatasaidia kutatua mzozo huo wala kuizuia Russia kufikia malengo yake.

XS
SM
MD
LG