Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:03

Tshala Muana mwanamuziki mashuhuri wa Congo amefariki


Wanamuziki kutoka Congo, marehemu Tshala Muana (K) akiwa na Koffi Olomide na Werrason
Wanamuziki kutoka Congo, marehemu Tshala Muana (K) akiwa na Koffi Olomide na Werrason

Alikuwa mwimbaji bora katika miaka ya 80 na 90 na nyimbo kama Dezo Dezo na Karibu Yangu ambazo zilitawala kwenye matangazo

Mwanamuziki mashuhuri wa Congo Elizabeth Tshala Muana Muidikayi maarufu kama jina la jukwaani Tshala Muana amefariki dunia Jumamosi asubuhi Desemba 10 jijini Kinshasa.

Kifo chake kilithibitishwa na mwenzake Claude Mashala katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.

"Mungu mwema ameamua kumchukua Mamu wa Taifa Tshala Muana. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote nzuri alizotuletea hapa duniani. Kwaheri Mamu kutoka kwangu," aliandika Mashala bila kueleza kwa undani sababu ya kifo chake.

Tshala Muana alikuwa na umri wa miaka 64 wakati wa kifo chake.

Alionekana kama "Malkia wa Mutuashi" muziki wa dansi wa kitamaduni kutoka mkoa wake wa asili wa Kasai, marehemu alishirikiana na wanamuziki wengine wa kizazi chake kuutangaza muziki wa Kongo kote ulimwenguni na ulijulikana kama "Mamu National".

Muimbaji huyu kutoka Kongo kwa muda mrefu afya yake haikuwa nzuri na hivi karibuni alilazwa hospitali kwa matibabu.

Alitoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba na alitumbuiza katika matamasha tofauti.

Alikuwa mwimbaji bora katika miaka ya 80 na 90 na nyimbo kama Dezo Dezo na Karibu Yangu ambazo zilitawala kwenye matangazo.

XS
SM
MD
LG