Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:38

Wanajeshi wawili wa Yemen wameuawa kwa shambulizi la kushtukiza


Mfano wa shambulizi la kwenye gari huko Yemen
Mfano wa shambulizi la kwenye gari huko Yemen

Kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa Ofisi ya Kimataifa ya Uhamiaji ya Umoja wa Mataifa wanajeshi hao wawili waliuawa wakati wakisindikiza msafara uliokuwa ukisafiri magharibi kutoka Seiyun kwenda Marib.

Wanajeshi wawili kutoka vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Yemen wameuawa katika shambulizi la kushtukiza kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Yemen, Umoja wa Mataifa umesema Jumamosi.

Kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa Ofisi ya Kimataifa ya Uhamiaji ya Umoja wa Mataifa, wanajeshi hao wawili waliuawa wakati wakisindikiza msafara uliokuwa ukisafiri magharibi kutoka Seiyun kwenda Marib. Hakuna mfanyakazi wa IOM, ambaye alikuwa katika operesheni ya kibinadamu ambayo haikutajwa, waliojeruhiwa katika shambulizi hilo, ilisema taarifa. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu tukio hilo la Ijumaa.

Kiongozi wa kikabila kutoka eneo hilo na afisa wa Umoja wa Mataifa wameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba uvamizi huo ulifanyika karibu na mji wa Al-Abr, katika jimbo la mashariki mwa Yemen la Hadhramout. Wote wawili walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao kutokana na hofu ya kulipiziwa kisasi.

Katika taarifa tofauti iliyotolewa Ijumaa na Luteni Jenerali Saleh Mohammed Timis wa Kikosi Maalum cha Yemen, tawi rasmi la jeshi linaloungwa mkono na Saudi Arabia watu hao wawili walitambuliwa kama Salem Saeed Qarwan na Salem Mubarak Al-Bahri.

XS
SM
MD
LG