Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:48

Equatorial Guinea inapiga kura Jumapili kumchagua Rais, Maseneta na Wabunge


Baadhi ya raia wa Eguatorial Guinea wanashiriki zoezi la upigaji kura siku ya Jumapili kumchagua rais, maseneta na wabunge nchini humo

Rais Teodoro Obiang mwenye umri wa miaka 80 ambaye anawania muhula mwingine amekuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 43 ikiwa ni uongozi mrefu zaidi wa kiongozi yeyote aliye madarakani hii leo isipokuwa kwa wafalme

Equatorial Guinea ilipiga kura Jumapili huku Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo akiwa na uhakika wa kushinda rekodi ya muhula wa sita katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku kukiwa hakuna upinzani wowote.

Obiang mwenye umri wa miaka 80 amekuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 43 ikiwa ni uongozi mrefu zaidi wa kiongozi yeyote aliye madarakani hii leo, isipokuwa kwa wafalme.

Wapiga kura kadhaa walikuwa tayari wamepanga foleni wakati milango ilipofunguliwa katika kituo cha kupigia kura kilichowekwa katika shule moja kwenye wilaya ya Semu huko Malabo mapema asubuhi kwa saa za huko.

"Upigaji kura unaendelea vizuri. Kila kitu kipo kama kawaida. Raia wote wanapaswa kupiga kura," mtu anaye fundi wa friji, Norberto Ondo aliliambia shirika la habari la AFP.

"Natarajia uchaguzi huu utatuletea mafanikio," aliongeza mpiga kura mwenye umri wa miaka 53 baada ya kuingiza kura yake kwenye sanduku katika shule ya Nuestra Senora de Bisila.

Kuchaguliwa tena kwa Obiang kunaonekana kuwa na uhakika katika mojawapo ya utawala wa ki-imla katika mojawapo ya nchi duniani.

Anayegombea dhidi yake ni Andres Esono Ondo, mwenye umri wa miaka 61, kutoka chama pekee cha upinzani kilichovumiliwa nchini humo.

Katibu mkuu wa chama cha Convergence for Social Democracy (CPDS) ni mgombea kwa mara ya kwanza na mwakilishi pekee wa upinzani unaokandamizwa.

Ondo amesema anahofia "wizi" wakati wa upigaji kura ili kumchagua rais, maseneta na wabunge.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG