Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:37

Uturuki imesema imefanya mashambulizi ya anga huko Syria na Iraq


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Wizara ya ulinzi ya uturuki imesema mashambulizi hayo yalipiga kambi za chama cha Kurdistan Workers (PKK) na Syrian People’s Protection Units (YPG). Washington inaunga mkono kundi la YPG katika vita vyake dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema Jumapili kwamba imefanya mashambulizi ya anga katika mikoa ya kaskazini mwa Syria na Iraq ambako wizara hiyo inayalenga makundi ya Kikurdi ambayo inaamini yanahusika na shambulizi la wiki iliyopita mjini Istanbul.

Wizara hiyo imesema mashambulizi hayo yalipiga kambi za chama cha Kurdistan Workers, au PKK, na Syrian People’s Protection Units au YPG.

Bomu lilipiga katikati mwa Istanbul wiki iliyopita na kuua watu sita na kujeruhi zaidi ya 80.

Uturuki inayalaumu PKK na YPG kwa shambulizi hilo, lakini makundi yote mawili yamekanusha mashtaka hayo.

Washington inaunga mkono kundi la YPG katika vita vyake dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.

XS
SM
MD
LG