Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:22

Nchi zimepitisha makubaliano magumu kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa


Wanaharakati nje ya mkutano wa COP27 huko Sharm el-Sheikh nchini Misri, Nov. 18, 2022.
Wanaharakati nje ya mkutano wa COP27 huko Sharm el-Sheikh nchini Misri, Nov. 18, 2022.

Wajumbe walipongeza mafanikio ya kuanzisha mfuko wa fedha kama haki ya hali ya hewa kwa lengo lake la kuzisaidia nchi zilizo katika mazingira magumu kukabiliana na dhoruba, mafuriko, na majanga mengine yanayochochewa na uzalishaji wa kihistoria wa kaboni unaofanywa na mataifa tajiri

Nchi zilipitisha makubaliano magumu ya mwisho katika mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa COP27 mapema Jumapili ambao unaanzisha mfuko wa kuzisaidia nchi maskini zilizokumbwa na majanga ya hali ya hewa lakini haiongezi juhudi za kukabiliana na uzalishaji unaosababisha hali hiyo.

Baada ya majadiliano makali yaliyoendelea usiku kucha, mwenyeji wa COP27 Misri ilitoa maandishi ya mwisho ya makubaliano na wakati huo huo kuitisha kikao cha jumla ili kulipitisha haraka suala hilo.

Uidhinishwaji wa haraka wa kuunda mfuko wa hasara na uharibifu wa kujitolea bado uliacha maamuzi mengi yenye utata juu ya mfuko huo hadi mwaka ujao, ikiwa ni pamoja na nani anapaswa kulipa.

Wapatanishi hawakuwa na pingamizi wakati Rais wa COP27 Sameh Shoukry alipopitisha haraka masuala yaliyokuwa kwenye ajenda ya mwisho. Na kufikia alfajiri wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wa kilele katika eneo la mapumziko la Sharm el-Sheikh nchini Misri leo Jumapili, makubaliano hayo yalifikiwa.

Licha ya kutokuwa na makubaliano ya kupunguza kwa viwango vikubwa uzalishaji wa gesi chafu, "tulikwenda na kile ambacho makubaliano yalikuwa hapa kwa sababu tunataka kusimama na walio hatarini zaidi," alisema waziri wa hali ya hewa wa Ujerumani Jennifer Morgan, huku akionekana kukasirika.

Wajumbe walipongeza mafanikio ya kuanzisha mfuko huo kama haki ya hali ya hewa, kwa lengo lake la kuzisaidia nchi zilizo katika mazingira magumu kukabiliana na dhoruba, mafuriko, na majanga mengine yanayochochewa na uzalishaji wa kihistoria wa kaboni unaofanywa na mataifa tajiri.

XS
SM
MD
LG