Jean Batiste Twisere kiongozi wa shirika la Kiraia la Jomba Chengerero eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23 ni miongoni mwa wanaopinga kujumuishwa kwa wapiganaji wa M23 katika jeshi la pamoja na serikali ya DRC baada ya mazungumzo.
Msimamo huo ukiwa miongoni mwa Vijana kutoka mikoa mbali mbali baada ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi kuomba vijana hao kujiunga na kusaidia jeshi kupambana na makundi ya waasi hasa kundi la 23. Ombeni Kasiano ni kutoka Mji wa Kiwanja naye amekimbia mji wake wa Kiwanja ambao kwa sasa upo mikoni mwa waasi wa M23.
Nao waasi hao wa M23 wamesema njia nzuri na bora ya kutatua mzozo huo wa mashariki mwa Congo ni mazungumzo kuliko kutumia nguvu. Wananchi wa eneo la waasi wa M23 wamesema hali ya kimaisha kwa sasa ni ngumu.
Wakati mazungumzo yanatarajiwa kufanyika kati ya M23 na serikali ya DRC, Nairobi Kenya Novemba 16 baada ya Mkutano uliofanyika Angola tarehe 5 ambapo Rwanda na Congo zimeombwa kutatua tofauti zao za Kidiplomasia.
Kwani wananchi wa kawaida wanaendelea na shughuli za kibiashara bila tatizo Goma Kivu Kaskazini na Bukavu Kusini.
Imeandaliwa na Austere Malivika VOA.