Muda mrefu wa maandalizi ya Kombe la Dunia la mwezi huu umeleta hali ya uchunguzi ambayo haikuwa imeshuhudiwa awali, kuhusu jinsi gani mamilioni ya wafanyakazi wa kigeni katika taifa la Uarabuni la Ghuba ambao walijenga viwanja na miundombinu mingine, na ambao watafanya kazi kwenye hoteli na kufagia barabara wakati wa michuano hiyo mikubwa zaidi ya michezo ulimwenguni.
Kutokana na ukosoaji mkubwa wa kimataifa, Qatar imepitisha mageuzi kadhaa katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuvunjwa kwa kiasi fulani sehemu ya mfumo uliowafunga wafanyakazi kwa waajiri wao na kuweka kima cha chini cha mshahara mabadiliko yaliyosifiwa na Umoja wa Mataifa pamoja na makundi ya haki za binadamu.
Lakini wanaharakati wanasema unyanyasaji kuanzia mishahara isiyolipwa hadi mazingira magumu ya kazi katika mojawapo ya nchi zenye joto kali Duniani, bado umeenea, na kwamba wafanyakazi ambao wamezuiwa kuunda vyama vyao au kugoma wana njia chache za uhakika za kufuata haki.
Pia wana wasiwasi kuhusu kitakachotokea baada ya mashindano hayo ya mwezi mzima kukamilika mwezi Desemba, wakati uangalizi wa kimataifa utakapoondoka na waajiri kupunguza mishahara yao.
Qatar inasema inaongoza kanda hiyo katika mageuzi ya ajira na kwamba mabadiliko hayo yataendelea baada ya Kombe la Dunia. Maafisa kutoka kwa Emiri mkuu anayetawala hadi chini wamewasema wakosoaji, wakiwashutumu kwa kupuuza mageuzi hayo na kulitenga isivyo haki taifa hilo la kwanza la Kiarabu au Kiislamu kuandaa Kombe hilo.
Qatar, kama nchi nyingine za Ghuba, inategemea mamilioni ya wafanyakazi wa kigeni, ambao ni idadi kubwa ya watu na karibu asilimia 95 ya nguvu kazi kutoka kwa watendaji wa makampuni wanaolipwa sana hadi wafanyakazi wa ujenzi.