Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 23:07

Rais Biden aahidi mswaada wa kwanza atakaoutuma bungeni mwaka ujao


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza wakati akihudhuria utiaji saini kuwa sheria Sheria ya Marekebisho ya Usafirishaji wa Meli ya 2022,

Rais Joe Biden anaahidi kwamba mswada wa kwanza atakaoutuma bungeni mwaka ujao utakuwa kuweka sheria dhidi ya ile ya Roe v. Wade ikiwa Wademokrat watadhibiti viti vya kutosha katika Bunge la Congress kwa Biden kutia saini ulinzi wa uavyaji mimba kuwa sheria.

Katika hotuba iliyoandaliwa kuwapa nguvu wapiga kura wa chama chake wiki tatu tu kabla ya uchaguzi wa katikati ya awamu wa Novemba, Biden alisema, "Ikiwa unajali haki ya kuchagua, basi unapaswa kupiga kura."

Wademokrat walijaribu mara kwa mara katika Bunge hili kusisitiza haki za uavyaji mimba kuwa sheria, na kuzuiwa na warepublikan kwa mfumo maalum bungeni uitwao Filibuster na kutokuwa tayari kwa wanachama wao kubadilisha sheria za Seneti.

Nguvu hiyo ina uwezekano wa kuendelea bila kujali kitakachotokea katika uchaguzi wa Novemba. Rais Biden alizungumza na wafuasi wa chama chake mjini Wahington jumanne.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG