Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:05

Papa Francis anasema kutengwa kwa wahamiaji ni "kashfa, karaha na dhambi"


Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki Duniani
Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki Duniani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis siku ya Jumapili alitoa utetezi mkali dhidi ya wahamiaji, akitaja kutengwa kwao kuwa "kashfa, karaha na dhambi", na kumuweka katika mgongano na serikali ijayo ya mrengo wa kulia ya Italia.

Papa Francis aliyasema hayo alipomsimika askofu wa karne ya 19 anayejulikana kama "baba wa wahamiaji" na mtu wa karne ya 20 ambaye alihudumia wagonjwa nchini Argentina.

Papa Francis, ambaye ameonyesha uungaji mkono wahamiaji kuwa mada kuu ya upapa wake, aliongoza sherehe hizo mbele ya watu 50,000 katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

"Kutengwa kwa wahamiaji ni kashfa. Hakika, kutengwa kwa wahamiaji ni kosa la jinai. Inawafanya wafe mbele yetu," alisema.

XS
SM
MD
LG