Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:31

Maelfu waandamana wakidai kupinga uchaguzi waliouita wenye dosari Angola


Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Angola UNITA, wanahudhuria mkutano wa mwisho wa chama huko Cazenga, nje ya mji mkuu wa Luanda nchini Angola, Agosti 22..REUTERS/Siphiwe Sibeko
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Angola UNITA, wanahudhuria mkutano wa mwisho wa chama huko Cazenga, nje ya mji mkuu wa Luanda nchini Angola, Agosti 22..REUTERS/Siphiwe Sibeko

Maelfu ya raia wa Angola waliandamana Jumamosi kupinga kile walichosema kuwa uchaguzi uliokuwa na dosari wa mwezi uliopita ambao ulikirejesha madarakani chama tawala cha MPLA baada ya takriban miongo mitano ya utawala.

Mahakama ya Katiba ya Angola ilitupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na chama cha upinzani UNITA, kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa Agosti 24.

Mahakama ya Katiba ya Angola ilitupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na mshindi wa pili, chama cha upinzani UNITA, katika uchaguzi wa Agosti 24.

UNITA, kundi la zamani la uasi ambalo lilipigana na chama tawala cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kwa takriban miongo mitatu, lilipata kura zake nyingi kutoka kwa vijana wanaohisi kuachwa nje ya utajiri wa mafuta nchini humo.

Waandamanaji waliimba kwa pamoja, “Wananchi hawako pamoja na MPLA. Tunataka waondoke!",.

Wengi wao walikuwa miongoni mwa vijana na wasio na ajira ambao wanahisi wameangushwa na MPLA, ambayo baadhi ya wanachama wake wamekuwa mabilionea kutokana na utajiri wa mafuta wa Angola huku wananchi walio wengi wanaishi katika umaskini.

Waandamanaji walikwenda uwanja wa Uhuru ambao kwa kawaida chama cha MPLA hufanya mikutano ya hadhara na hafla ya ushindi. Maandamano hayo yalikuwa ya amani, ingawa wachambuzi wanahofia kuna hasira ya kutosha na vijana kukerwa sana na hali ya maisha na kusababisha mambo kuweza kubadilika mara moja na kuwa ghasia.

XS
SM
MD
LG