Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:03

Wanajeshi watatu wa Ivory Coast wameachiwa huru kutoka nchini Mali


Mfano wa wanajeshi wa Ivory Coast
Mfano wa wanajeshi wa Ivory Coast

Wanajeshi watatu wa kike wa Ivory Coast waliwasili nchini kwao mwishoni mwa wiki baada ya kuzuiliwa kwa takribani miezi miwili nchini Mali huku wengine 46 wakiwa bado wako gerezani katika kesi ambayo imeongeza mivutano kati ya majirani hao wa Afrika magharibi.

Waziri wa mambo ya nje wa Togo, Robert Dusse ambaye nchi yake imekuwa mpatanishi wa mazungumzo alisema wanawake hao watatu waliachiliwa kama ishara ya kibinadamu na kiongozi wa Mali, Kanali Assimi Goita. Tuna huzuni kwa sababu marafiki zetu bado wako huko na tunatarajia kujumuika nao hivi karibuni, alisema mmoja wa wanajeshi hao, Sita Bamba, ambaye aliachiliwa huru pamoja na Awa Bakayoko na Kangah Badou Adele Bledou.

Wanajeshi hao wa Ivory Coast walitumwa Mali mwezi Julai kufanya kazi katika Sahelian Aviation Services, kampuni ya binafsi iliyopewa kandarasi na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo serikali ya Mali ilisema inawachukulia raia hao wa Ivory Coast kuwa mamluki kwa sababu hawakuajiriwa moja kwa moja na tume ya Umoja wa Mataifa na kuwafungulia mashtaka ya kuhujumu usalama wa taifa.

Mamlaka ya Mali ilisema kampuni hiyo ya usafiri wa anga inapaswa kuanzia sasa kukabidhi masuala ya usalama wake kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Mali.

XS
SM
MD
LG