Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 15:54

Meli ya kivita ya Uturuki imetia nanga Israil baada ya zaidi ya muongo mmoja


Mfano wa meli ya kivita ya uturuki iliyotia nanga huko Israel katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja
Mfano wa meli ya kivita ya uturuki iliyotia nanga huko Israel katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja

Meli ya kivita ya Uturuki imetia nanga huko Israel kwa ziara ya kwanza ya aina hiyo katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja huku uhusiano kati ya washirika wa Marekani ukiimarika kufuatia mvutano mkali kuhusu wa-Palestina.

Meli ya Kemal Reis ilitia nanga Jumamosi kama sehemu ya ujanja wa NATO katika bahari ya Mediterranean afisa wa Uturuki alisema. Afisa mmoja wa Israel alisema Ankara imewasilisha ombi la awali la kuwataka wafanyakazi hao kuondoka pwani.

Afisa katika bandari ya Haifa amesema hii ni mara ya kwanza kwa meli ya kijeshi ya Uturuki kutembelea huko tangu angalau mwaka 2010 wakati uhusiano wa pande mbili ulipovunjwa na hatua ya Israel kuuvamia msafara wa makundi ya misaada yanayoiunga mkono Palestina ambayo ilijaribu kukiuka vizuizi vyake vya ukanda wa Gaza.

Watu 10 waliuawa na jeshi la majini la Israel katika tukio hilo. Kwa upande wake Israel imeeleza pingamizi dhidi ya Uturuki yenye uanachama wa NATO kuwakaribisha wanachama wa Hamas vuguvugu la kiislam ambalo linatajwa kama kundi la kigaidi katika nchi za magharibi.

XS
SM
MD
LG