Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:13

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko nchini Pakistan inaongezeka


Mafuriko ynaendelea nchini Pakistan yanayodaiwa kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko makubwa nchini Pakistan iliendelea kuongezeka siku ya Jumamosi kukiwa na vifo 57 zaidi ambapo watu 25 kati yao ni watoto huku nchi hiyo ikikabiliana na operesheni za misaada pamoja na uokoaji kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Chombo cha ngazi ya juu kilichoundwa kuratibu juhudi za misaada kilikutana mjini Istanbul siku ya jumamosi kwa mara ya kwanza kikiongozwa na Waziri Mkuu Shehbaz Sharif kutathmini maafa hayo.

Rekodi za mvua na barafu inayoyeyuka katika milima ya kaskazini ilileta mafuriko ambayo yameathiri watu milioni 33 na kuua takribani watu 1,265 wakiwemo watoto 144.

Mafuriko hayo yanayolaumiwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa bado yanaenea kusambaa. Idadi ya vifo vya watoto imezua wasiwasi. Siku ya Ijumaa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) lilisema kulikuwa na hatari ya vifo vya watoto wengi kutokea kutokana na mafonjwa baada ya mafuriko hayo.

XS
SM
MD
LG