Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:28

Emirates yaanza tena safari za ndege kuelekea Nigeria


Nigeria Emirates Flights Suspension
Nigeria Emirates Flights Suspension

Emirates itaanza tena safari za ndege kuelekea Nigeria mwezi huu baada ya Benki Kuu ya Nigeria kulipa  sehemu ya fedha ambazo shirika la ndege la Dubai lilikuwa limepata nchini humo lakini hawakurejeshewa.

Msemaji wa shirika la ndege alisema safari za ndege kwenda Lagos zitaanza tena Septemba 11, ingawa haiwezekani kurejesha safari za kuelekea Abuja mwezi Septemba kwa sababu rasilimali tayari zimesimamishwa.

"Tunaendelea kushirikiana na mamlaka ya Nigeria ili kuhakikisha urejeshaji wa fedha zetu ambazo bado hazijalipwa na zinazokuja unaweza kuendelea bila pingamizi," msemaji huyo alisema, akikaribisha kile ilichokisema kuwa ni hatua ya benki kuu ya kutoa sehemu ya fedha zake zilizozuiwa.

XS
SM
MD
LG