Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:52

Ripoti ya UN ya maendeleo endelevu 2022 inaonya matatizo yatakayozuia kufikiwa malengo yao 2050


Ripoti ya malengo na maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa
Ripoti ya malengo na maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa

Ripoti ya malengo na maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022 inaonya matatizo na majanga ya ulimwengu yanaweka hatarini kufikiwa ifikapo mwisho wa muongo wa malengo 17 yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa hapo mwaka 2015.

Taarifa katika ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii kutoka zaidi ya nchi 200 zinaonyesha kuwa COVID-19, mabadiliko ya hali ya hewa, na mizozo inayozidi kusambaa yana athari kubwa katika juhudi za kumaliza umaskini na njaa pamoja na kuboresha afya na usalama duniani.

Mkurugrnzi msaidizi wa kitengo cha takwimu cha Umoja wa Mataifa Francesca Perucci anasema COVID-19 imefuta zaidi ya miaka minne ya maendeleo katika kupunguza umaskini. Anasema janga hilo limesukuma watu milioni 93 katika umaskini uliokithiri na wengi zaidi kuingia katika njaa kali.

Anasema kuongezeka kwa idadi hiyo na kuenea kwa mizozo duniani ambapo ni janga kubwa zaidi tangu mwaka 1946, kumelazimisha zaidi ya watu milioni 100 kutoka kwenye nyumba zao.

“Mgogoro wa Ukraine umesababisha bei ya chakula, mafuta na mbolea kupanda sana, na kuvuruga usambazaji na biashara ya kimataifa, soko la fedha limedorora na kutishia usalama wa chakula na mtiririko wa misaada duniani. Hali ya kibinadamu pia iko kwenye hati-hati ya janga la hali ya hewa na athari ambazo tayari zinashuhudiwa na kugusa mamilioni ya watu ulimwenguni kote”.

Wanasayansi wanasema uzalishaji wa gesi chafu uliongezeka kwa rekodi ya asilimia sita mwaka jana. Ili kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya hali ya hewa wanasema uzalishaji wa Carbon Dioxide lazima uwe juu kabla ya mwaka 2025, na kushuka kwa asilimia 43 ifikapo mwaka 2030 na kushuka hadi sifuri ifikapo mwaka 2050.

Wanasayansi wanaonya ahadi za kitaifa za hiari za kupunguza utoaji wa gesi chafu hautoshi kufikia lengo hili. Badala yake wanasema ahadi hizo zitasababisha kuongezeka kwa karibu asilimia 14 katika uzalishaji wa CO2 katika muongo ujao.

XS
SM
MD
LG