Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:45

Ukraine imepandisha bendera yake kwenye Kisiwa cha Snake ikionyesha ukaidi kwa Russia


Snake Island kipo takribani kilomita 140 kusini mwa Ukraine
Snake Island kipo takribani kilomita 140 kusini mwa Ukraine

Ukraine ilipandisha bendera yake ya bluu na njano kwenye kisiwa cha Snake katika Black Sea hapo Alhamis ikionyesha ukaidi lakini Russia ilijibu haraka kwa shambulizi lililoharibu sehemu ya kituo hicho cha Ukraine.

Udhibiti wa kisiwa hicho kilichopo takribani kilomita 140 kusini mwa Ukraine katika bandari ya Odesa umekuwa na mzozo tangu Rais wa Russia Vladimir Putin alipoivamia Ukraine zaidi ya miezi mine iliyopita.

Katika siku za mwanzo za vita Russia ilikishambulia kisiwa hicho baada ya wanajeshi wa Ukraine kujibu kwa maneno machafu wakati mabaharia wa meli ya kivita ya Moskva walipowataka wajisalimishe. Ukraine ilitoa muhuri wa ukumbusho kusheherekea ukaidi wa wanajeshi.

Russia ilikuwa imekidhibiti kisiwa hicho kwa muda mwingi wa vita hivyo hadi Ukraine ilipokikamata tena kisiwa hicho wiki iliyopita ingawa Russia ilisema kuwa iliondoka kama ishara ya nia njema.

XS
SM
MD
LG