Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 06:34

Watu 19 wamefariki Ivory Coast kutokana na mvua kubwa zinazonyesha nchini humo


Mvua kubwa nchini Ivory Coast zimesababisha maafa na uharibifu wa miundombinu mbalimbali

Watu 19 wamefariki nchini Ivory Coast mwezi huu baada ya mvua nyingi kunyesha katika mji mkuu wa kiuchumi wa Abidjan ambao umekumbwa na msimu wa mvua nyingi ofisi ya rais ilisema Alhamis.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa baraza la usalama la kitaifa kutangaza idadi ya kusikitisha ya watu 19 waliofariki, watano walijeruhiwa pamoja na uharibifu mkubwa wa mali katika wilaya kadhaa za Abidjan.

Mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili ilipiga Abidjan Juni 16 na 22 na kusababisha mafuriko na maporomoko makubwa ya ardhi. Rais wa Ivory Coast Alasane Ouattara baada ya kubainisha kuwa Ivory Coast kama nchi nyingi duniani inakabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa, amewasihi wakaazi kuondoka katika maeneo yenye hatari ilisema taarifa hiyo.

Operesheni ya kuhamisha watu katika maeneo yapatayo 50 yanayotishiwa na maporomoko ya ardhi ilizinduliwa mapema mwezi Juni wakati msimu wa mvua ukianza nchini Ivory Coast.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG