Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 13:39

Marekani imeweka vikwazo kwa makampuni inayoyashutumu kuuza petroli ya Iran


Marekani imeweka vikwazo dhidi ya makampuni inayoyashutumu kusaidia kupeleka na kuuza petroli ya Iran
Marekani imeweka vikwazo dhidi ya makampuni inayoyashutumu kusaidia kupeleka na kuuza petroli ya Iran

Marekani siku ya Jumatano iliweka vikwazo dhidi ya mtandao wa Hong Kong, Umoja wa Falme za Kiarabu, na makampuni mengine ambayo inayashutumu kusaidia kupeleka na kuuza petroli ya Iran na bidhaa za petroli kwa nchi za Asia mashariki ikiiwekea shinikizo Tehran wakati Washington inataka kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015.

Wizara ya hazina ya Marekani ilisema katika taarifa yake kuwa mtandao wa watu na mashirika ulitumia mtandao wa makampuni yenye makazi yake katika nchi za Ghuba ya Uajemi kuwezesha usafirishaji na uuzaji wa bidhaa zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dola kutoka kwa makampuni ya Iran hadi Asia ya Mashariki.

Mjini Doha wiki iliyopita mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington yalimalizika bila mafanikio kuhusu jinsi ya kuokoa mkataba wa nyuklia ya Iran yam waka 2015.

Miongoni mwa waliotajwa kuwekewa vikwazo Jumatano ni kampuni ya Jam Petrochemical Co, yenye makao yake nchini Iran ambayo Washington iliishutumu kwa kusafirisha bidhaa za kemikali zinazotokana na petroli kwa makampuni yote Asia mashariki ambayo mengi yaliuzwa kwa Iran Petrochemical Commercial Co.

XS
SM
MD
LG