Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:53

Mjumbe wa UN nchini Sudan Kusini anaelezea wasiwasi kuhusu utekelezaji wa mkataba wa amani


Nicholas Haysom, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini
Nicholas Haysom, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini alielezea wasi wasi wake Alhamis kwamba muda unazidi kuyoyoma kwa utekelezaji kamili wa makubaliano ya Amani ya nchi hiyo.

Wapinzani wa kisiasa wa Sudan Kusini walitia saini makubaliano hayo mwaka 2018 lakini bado wanashindwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda wa miaka mitano ambavyo vimesababisha karibu watu laki nne kuuawa katika nchi hiyo change zaidi duniani. Nicholas Haysom mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambae pia ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) anasema wasiwasi wake mkuu ni kwamba mwisho wa kipindi cha mpito unakaribia kwa kasi lakini maendeleo katika utekelezaji wa makubaliano ya Amani yamekuwa ya polepole.

Aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Juba ikiwa imesalia miezi minane pekee fursa ya kutekeleza vigezo muhimu inatoweka akitoa wito kwa viongozi hao hasimu kufikia maridhiano yanayohitajika.

XS
SM
MD
LG