Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 00:45

Tume ya haki za binadamu Ethiopia inatoa wito wa kuachiliwa watu waliokamatwa huko Tigray


EHRC na EHRCO ni tume zinazoangazia masuala ya haki za binadamu nchini Ethiopia

Tume ya haki za binadamu ya Ethiopia (EHRC) ilitoa wito Jumatano kuachiliwa mara moja kwa zaidi ya watu 8,500 kutoka mkoa unaokumbwa na vita wa Tigray ambapo inasema wanazuiliwa kinyume cha sheria katika kambi mbili.

EHRC ilisema wanaume, wanawake na watoto 8,560 walioko huko walikamatwa kinyume cha sheria na kiholela kwa misingi ya utambulisho wao wa kikabila na kuzuiliwa huko tangu Disemba. Kambi hizo mbili zilikuwa Semera kwenye mji mkuu wa mkoa wa Semera unaopakana na Tigray ilisema EHRC ambayo ni taasisi ya umma yenye hadhi maalum.

Familia zilikuwa zimefarakana huku wanaume na wanawake wakitenganishwa iliongeza taarifa hiyo. Watu kadhaa walikufa kwa magonjwa kwa sababu huduma za matibabu na misaada ya kibinadamu katika kambi hizo zilikuwa chache mno. Watu waliozuiliwa kwenye kambi walikatazwa kwenda kwenye vituo vya afya isipokuwa kwa wanawake wanaojifungua ilisema tume ya haki za binadamu ya Ethiopia (EHRC).

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG