Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:20

Zaidi ya watu 100 wengi wanawake wameuawa nchini Syria


Kambi ya Al-Hol nchini Syria ambayo wakaazi wengi ni wanawake na watoto waliokamatwa baada ya kukimbia mapigano dhidi ya kundi la Islamic State. Oct. 20, 2021. (Ali Zeyno/VOA)
Kambi ya Al-Hol nchini Syria ambayo wakaazi wengi ni wanawake na watoto waliokamatwa baada ya kukimbia mapigano dhidi ya kundi la Islamic State. Oct. 20, 2021. (Ali Zeyno/VOA)

Zaidi ya watu 100 wengi wao wakiwemo wanawake wameuawa kwenye kambi moja nchini Syria katika muda wa miezi 18 pekee Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne ukizitaka nchi kuwarejesha makwao raia wao.

Kambi ya Al-Hol inazidisha hofu ya kutokuwa na usalama na watoto wanaokamatwa wanahukumiwa maisha alisema Imran Rizi mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria.

Al-Hol iliyoko kaskazini-mashariki inadhibitiwa na wa-Kurd ilikusudiwa kuwa kituo cha muda cha kushikilia watu. Hata hivyo bado inawashikilia takribani watu 56,000 wengi wao wakiwa wa Syria na wa Iraq ambao baadhi yao wana uhusiano na kundi la wapiganaji wa Islamic State ambalo liliteka maeneo mengi ya Iraq na Syria hapo mwaka 2014.

Wengine ni raia wa nchi nyingine wakiwemo watoto na jamaa wengine wa wapiganaji wa IS. Asilimia 94 ya wafungwa ni wanawake na watoto Rizi ambaye ametembelea Al-Hol mara kadhaa aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

XS
SM
MD
LG