Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:15

Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia Hamadi Jebali ameachiwa huru lakini anaendelea kuchunguzwa


Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia, Hamadi Jebali ameachiwa huru lakini anaendelea kuchunguzwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha
Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia, Hamadi Jebali ameachiwa huru lakini anaendelea kuchunguzwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha

Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia na afisa mkuu wa chama cha Ennahdha chenye kufuata misingi ya kiislam, Hamadi Jebali aliachiliwa huru siku ya Jumatatu ikiwa ni siku ya nne baada ya kukamatwa kwake, mmoja wa mawakili wake alisema.

Jaji aliamuru kuachiliwa kwa Jebali lakini bado anachunguzwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha, wakili Samir Dilou aliliambia shirika la habari la AFP.

Atalazimika kufika mahakamani Julai 20 mbele ya jaji wa kitengo cha kupambana na ugaidi cha Tunis, Dilou aliongeza. Akiwa katika mgomo wa kula tangu kukamatwa kwake Jebali alilazwa hospitali Jumamosi akiwa kizuizini walisema mawakili wake.

Jebali alikamatwa Alhamis huko Sousse mji wa pwani kusini wa mji mkuu wa Tunis kwa tuhuma za utakatishaji fedha kupitia usafirishaji wa fedha za kigeni kwa shirika la misaada nchini Tunisia kulingana na wizara ya mambo ya ndani.

Hata hivyo Jebali anakanusha mashtaka hayo na anasema kwamba ukamataji huo ulikuwa sehemu ya kampeni ya kusuluhisha matokeo ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG