Kampuni ya nishati ya Sonatrach ya serikali ya Algeria siku ya Jumatatu ilitangaza ugunduzi wa akiba muhimu ya gesi katika uwanja wa Hassi R’mel katika jangwa la Sahara.
Taarifa ya Sonatrach inaeleza kwamba imegundua uwezekano mkubwa wa mafuta ghafi katika uwanja wa uchimbaji mafuta wa Hassi R’mel. Taarifa inaeleza kwamba Akiba hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango cha gesi ghafi cha karibu metric za mraba bilioni 100 hadi 340.
Kiwango hiki ni mojawapo ya kiwango kikubwa zaidi cha akiba kilichogunduliwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Sonatrach inapanga kuanza kufanya kazi ya uchimbaji kwenye uwanja huo kuanzia mwezi Novemba huku uzalishaji ukitarajiwa kufikia mita za ujazo milioni 10 kwa siku.
Algeria imethibitisha kuwa na akiba ya gesi asilia ya takribani metric za mraba trilioni 2.4 na kuipatia ulaya takribani asilimia 11 ya gesi yake inayoagizwa kutoka nje.