Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:04

Mafanikio ya kulinda mazingira kutokana na kazi za kibinadamu yamepatikana; inasema CBD


Ukataji misitu ni mojawapo ya uharibifu wa mazingira duniani
Ukataji misitu ni mojawapo ya uharibifu wa mazingira duniani

Wajumbe kutoka takribani mataifa 200 wamepiga hatua kidogo kuelekea kuandaa rasimu ya mkataba wa kimataifa wa kulinda mazingira kutokana na kazi za kibinadamu baada ya karibu wiki nzima ya mazungumzo magumu mjini Nairobi.

Mikutano hiyo iliyohitimishwa Jumapili ililenga kuondoa tofauti miongoni mwa wanachama 196 wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya mchanganyiko wa viumbe(CBD) ikiwa ni takribani miezi sita kabla ya mkutano muhimu wa COP-15 mwezi Disemba.

Lengo kuu ni kuandaa rasimu ya maandishi inayoelezea mfumo wa kimataifa wa kuishi kwa kupambana na mazingira asili ifikapo mwaka 2050 na malengo makuu yatafikiwa ifikapo mwaka 2030.

Wengi wanatumai mpango huo wa kihistoria utakapokamilika utakuwa na malengo makubwa ya kulinda maisha duniani kama vile ulivyokuwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa ya mwisho ya vyombo vya habari kutoka CBD ilisema wajumbe wamefikia makubaliano juu ya malengo kadhaa. Elizabeth Maruma Mrema katibu mtendaji wa CBD alikiri wakati akifunga mkutano na waandishi wa habari kwamba maendeleo yalikuwa kidogo lakini aliongeza kuwa hawawezi kukubali kushindwa.

Kuna kazi nyingi zaidi ya kile walichofikiria alisema Basile van Havre mwenyekiti mwenza wa CBD. Lakini aliongeza kwamba kazi hiyo inawezekana.

XS
SM
MD
LG