Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 01:18

Beijing iko tayari kusaidia Pembe ya Afrika kupata amani; anasema Xue Bing


 Xue Bing ni mjumbe maalum wa China kwa Pembe ya Afrika akizungumza kwenye mkutano Addis Ababa, Ethiopia. June 20, 2022.
Xue Bing ni mjumbe maalum wa China kwa Pembe ya Afrika akizungumza kwenye mkutano Addis Ababa, Ethiopia. June 20, 2022.

Mjumbe maalum wa China kwa pembe ya Afrika, Xue Bing amesema Beijing iko tayari kuzisaidia nchi za eneo hilo kupata amani na kuondokana na kile alichokiita uingiliaji wa nje. Xue alitoa maoni hayo kwenye mkutano wa kwanza wa China juu ya utawala na maendeleo katika pembe ya Afrika unaofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Katika mkutano na nchi sita za Pembe ya Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa siku ya Jumatatu, China ilieleza kuwa machafuko na mgawanyiko wa kikanda unaongezeka.

Xue Bing, mjumbe maalum wa China kwa pembe ya Afrika alieleza kwamba fikra za vita baridi na madaraka ya kisiasa yameibuka tena, huku Amani na maendeleo vikikabiliwa na upinzani.

Ingawa China imekuwa mshirika wa muda mrefu wa kibiashara barani Afrika, hii ni mara ya kwanza inaonekana kuingilia kati siasa za nchi za kiafrika,-mabadiliko ya sera ya China.

Xue anasema mapema mwaka huu, mtazamo wa China kuhusu Amani na maendeleo ya Pembe ya Afrika ulizingatia hali halisi ya eneo hilo, na uzoefu wake wa siku za nyuma na unalenga kuzisaidia nchi za eneo hilo, kuondokana na uingiliaji kati kutoka nje. “China itaendelea kuunga mkono nchi za kanda hiyo ili kuzingatia maono ya usalama wa pamoja wa kina, wa ushirikiano na endelevu. Kulinda Amani na usalama wa kikanda pamoja na kunyamazisha bunduki katika Pembe ya Afrika”.

Balozi Redwan Hussein, mshauri wa usalama wa taifa wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, alieleza kuwa nchi za Pembe ya Afrika zinahitaji kutumia mbinu tofauti, kutatua changamoto za umaskini, ukame, uhamiaji haramu na wakimbizi, ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa, watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi, pamoja na matokeo ya vita.

“Uhusiano kati ya Amani na usalama ni Dhahiri sana kuweza kufafanuliwa hapa. Kulifanya eneo hilo kuwa huru kutokana na mzigo wa vita na migogoro pamoja na kuhakikisha amani na usalama vinaendelea kuwa kipaumbele cha pande zote. Watu wa eneo hilo wameteseka vya kutosha, na ni wajibu kwetu kuamua njia ya kistaarabu, iliyokomaa ya kushughulikia matatizo na tofauti zetu”.

China imesisitiza kuwa kwa muda mrefu imekuwa na Imani kwamba nchi za Pembe hiyo zina azimio muhimu la kutafuta nguvu kupitia mshikamano na busara ya kisiasa ili kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano.

XS
SM
MD
LG