Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:21

Raia takribani 100 wameuawa kaskazini mwa Burkina Faso; vyanzo vya usalama vimesema


Ramani ya Burkina Faso na nchi zilizo jirani
Ramani ya Burkina Faso na nchi zilizo jirani

Watu wenye silaha waliwaua takribani raia 100 katika wilaya ya mashambani kaskazini mwa Burkina Faso karibu na mpaka na Niger mwishoni mwa wiki chanzo cha usalama kilisema.

Washambuliaji waliwalenga wanaume lakini walionekana kuwaachia wanawake na watoto katika wilaya ya Seytenga Jumamosi usiku chanzo cha usalama na vyanzo vingine viwili vilisema wote wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi lakini inaelezea shambulizi hilo lilitokea katika maeneo ya mpakani ambako wanamgambo wanaohusishwa na al-Qaida na Islamic State wanaendesha uasi wao huko.

Takribani watu 3,000 waliokimbia shambulizi hilo wamewasili Dori mji mkuu wa Burkina Faso katika eneo la Sahel ambako mashirika ya misaada yapo kwenye eneo alisema afisa wa eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Kulikuwa na taarifa tofauti juu ya idadi ya vifo. Afisa huyo wa usalama alisema siku ya Jumatatu kwamba takribani watu 100 walikufa. Chanzo katika eneo hilo ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema kwamba idadi ya watu waliokufa ilikuwa 165.

XS
SM
MD
LG