Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:58

Rais Zelenskyy ajivunia Waukraine kuwarudisha nyuma warussia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa kwenye handaki Desemba 6,2021 .(AP).
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa kwenye handaki Desemba 6,2021 .(AP).

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anasema hakuna anayejua vita nchini mwake vitadumu kwa muda gani lakini vikosi vya Ukraine vinakaidi matarajio ya Russia kwa kuwazuia wanajeshi wa nchi hiyo kuvuka mashariki mwa Ukraine.

Katika hotuba yake ya video ya Jumamosi usiku , Zelenskyy alisema anajivunia Waukraine kuwarudisha nyuma warussia katika mkoa wa Donbas. "Kumbuka jinsi huko Russia mwanzoni mwa Mei, walitarajia kuikamata Donbas yote?" rais aliuliza kwa kejeli Jumamosi usiku.

Baada ya kushindwa kuikamata Kyiv, mji mkuu wa Ukraine, Moscow imejikita katika kuteka sehemu za eneo la mashariki lisiloshikiliwa na watu wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Moscow. Lakini badala ya kupata udhibiti wa haraka, vikosi vya Russia vimekabiliwa na vita vikali.

XS
SM
MD
LG