Tume ya Umoja wa Ulaya ilisema Jumatano kwamba Croatia ilitimiza vigezo vyote vya kujiunga na ukanda wa ulaya na hivyo kufungua njia kwa nchi hiyo kuwa mwanachama wa 20 kutumia sarafu moja hapo Januari mosi.
Croatia kubadili sarafu yake na kwenda Euro itakuwa chini ya muongo mmoja baada ya Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia ilipojiunga na Umoja wa Ulaya na kuweka hatua mpya katika ushirikiano zaidi wa umoja huo.
Afisa mkuu wa EU alisema Croatia ilitimiza masharti magumu ya kuwa sehemu ya sarafu moja ikiwa ni pamoja na kuweka mfumuko wa bei katika kiwango sawa na wenzao wa EU na pia kukumbatia matumizi ya umma.
Kujiunga na sarafu moja kutafanya uchumi wa Croatia kuwa na nguvu na kuleta manufaa kwa raia wake, wafanyabiashara, na jamii kwa jumla, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alisema. Kuipitisha Croatia kutumia sarafu ya Euro kutaifanya euro kuwa na nguvu zaidi aliongeza von der Leyen.