Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:31

Biden na Jacinda Arden wameshauriana juu ya udhibiti wa bunduki na itikadi kali za mtandaoni


Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern katika Oval Office huko White House. May 31, 2022.
Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern katika Oval Office huko White House. May 31, 2022.

Rais Joe Biden alimwomba ushauri Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden siku ya Jumanne baada ya ufyatuaji risasi wa umma wa hivi karibuni nchini Marekani lakini White House pia ilikiri mapungufu inayokabiliana nayo katika udhibiti wa bunduki ikilinganishwa na washirika wake wa karibu.

Katika mkutano na Arden huko Oval Office, Biden alielezea mauaji ya mwaka 2019 ya Christchurch ya watu 51 katika ufyatuaji risasi wa umma uliowalenga waislam. Umwagaji damu huo ulisababisha New Zealand kupiga marufuku bunduki za kijeshi na kuanzisha mchakato uliofanikiwa juu ya ununuzi wa bunduki.

“Tunahitaji muongozo wako” Biden alisema akimaanisha ushirikiano mpana wa Marekani na New Zealand lakini hasa kwa kile alichokiita juhudi za kimataifa za kukabiliana na vurugu na itikadi kali za mtandaoni. Nataka kufanya kazi nanyi katika juhudi hizo aliongeza.

Biden ambaye aliutembelea mji wa Uvalde kwenye jimbo la Texas siku ya Jumapili kuomboleza vifo vya watoto 19 na waalimu wawili waliouawa na mtu mwenye bunduki akitumia bunduki ya kijeshi alisema kulikuwa na mateso mengi na kwamba mengi ya hayo yanaweza kuzuilika.

XS
SM
MD
LG