Mazoezi ya Japan na Marekani, yalihusisha ndege nane za vita ambazo zipo Japan, ikiwemo ndege nne za Marekani F-16 na nne za Japan F-15.
Mazoezi hayo ya pamoja yamelenga kudhibitisha uwezo wa kijeshi wa pamoja wa nchi hizo mbili, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Japan na Marekani.
Mazoezi hayo yamefanyika saa chache baada ya Korea kaskazini kurusha makombora matatu, ikiwemo kombora la masaa marefu kuelekea katika habari iliyo kati ya Peninsula ya Korea na Japan.
Kuna wasiwasi kuhusu majaribio ya silaha za nuclear za Korea Kaskazini.
Makombora yalianguka baharini, nje ya eneo la kiuchumi la Japan.
Ndege za kurusha mabomu za China na Russia nazo zilifanya mazoezi karibu na Japan, jumanne wakati rais wa Marekani Joe Biden alikuwa anakutana na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida na washirika wao kutoka India na Australia kujaidli ushirikiano wa kiusalama, na uchumi.