Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 03:47

Marekani inawakaribisha viongozi wa Amerika Kusini kwenye mkutano wa bara la Amerika


Rais wa Marekani, Joe Biden
Rais wa Marekani, Joe Biden

Marekani ilisema Jumatatu inatafuta njia za kuwawakilisha watu wa Cuba, Venezuela na Nicaragua katika mkutano wa kilele mwezi ujao kufuatia vitisho vya kususia kutengwa kwa serikali zao.

Marekani inawakaribisha viongozi wa Amerika Kusini mjini Los Angeles kwa ajili ya mkutano wa bara la Amerika kuanzia June 6 hadi 10 ikiwa ni sehemu ya juhudi za Rais Joe Biden kuhamasisha demokrasia na kukabiliana na uhamiaji, pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Maafisa wa marekani walisema kwamba waliyataarifu rasmi mataifa hayo wiki iliyopita , na kwamba mialiko zaidi itafuata.

“Bado tunatathmini chaguo la namna ya kujumuisha vyema sauti za watu wa Cuba, Venezuela na Nicaragua katika mchakato wa mkutano huo” afisa katika utawala alisema.

Wizara ya mambo ya nje hapo awali, ilielezea Imani katika ushiriki imara huko Los Angeles bila ya kufichua orodha ya mwaliko.

Afisa wa cheo cha juu kwa Latin America, Brian Nicols awali alisema hatarajia mialiko kwa maafisa kutoka Cuba, Nicaragua, na Venezuela kwa vile serikali zao haziheshimu mkataba wa mwaka 2001 wa Inter-American Democratic Charter.

Lakini Cuba ilialikwa kwenye mikutano ya kilele hapo mwaka 2015 huko panama na mwaka 2018 huko Peru. Tangu wakati huo Biden amekuwa akifanya mabadiliko ya mtangulizi wake Donald Trump kwa Marekani kufungua tena shughuli zake kwenye kisiwa hicho kinachoendeshwa kikomunisti.

Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador ambaye ni mrengo wa kushoto anatishia kususia mkutano huo kama Marekani haitazialika nchi zote.

Tangu wakati huo viongozi wa Argentina, Bolivia, Honduras na Jumuiya ya Mataifa 14 ya Caribbean pia wameweka ushiriki wao mashakani huku Chile ikijiunga na wito kwa uwezekano mkubwa wa kushiriki.

XS
SM
MD
LG