Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 12:08

Russia inasema jumla ya wanajeshi 1,730 wa Ukraine wamejisalimisha wiki hii


Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano. May 8, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano. May 8, 2022.

Wizara ya ulinzi ya Russia ilisema Alhamis kwamba mamia ya wanajeshi wa Ukraine wamejisalimisha katika kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa huko Mariupol na kufanya jumla ya wanajeshi 1,730 waliojisalimisha wiki hii.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) ilisema katika taarifa yake ilikuwa ikiwasajili wapiganaji ambao waliondoka Azovstal operesheni iliyoanza Jumanne na iliendelea Alhamis.

ICRC haisafirishi POWs kuelekea mahala ambapo wanashikiliwa kundi hilo la misaada lilisema. Mchakato wa usajili ambao ICRC iliusimamia unahusisha mtu kujaza fomu yenye maelezo ya kibinafsi kama vile jina, tarehe ya kuzaliwa, na ndugu wa karibu. Taarifa hizi zinairuhusu ICRC kuwafuatilia watu ambao wamekamatwa na kuwasaidia kuwasiliana na familia zao.

XS
SM
MD
LG