Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:57

Kiongozi wa Taliban nchini Afghanistan anaahidi nchi hiyo haitakuwa tena tishio kwa Marekani


Kaimu Naibu wa mambo ya ndani nchini Afghanistan Sirajuddin Haqqani
Kaimu Naibu wa mambo ya ndani nchini Afghanistan Sirajuddin Haqqani

Kiongozi wa cheo cha juu wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan anaahidi nchi yake kamwe haitakuwa tena tishio la kigaidi kwa Marekani na aliahidi habari njema hivi karibuni juu ya kurejea kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan katika shule za sekondari. Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Sirajuddin Haqqani pia Naibu Mkuu wa Taliban alisisitiza tena uhakikisho huo katika mahojiano nadra na Christiane Amanpour wa CNN yaliyotangazwa Jumatatu.

Kundi la Taliban lilipata tena mamlaka baada ya wanajeshi wa Marekani na NATO kujiondoa katika taifa hilo la Asia Kusini lililokumbwa na vita hapo Agosti mwaka 2021 na lilianzisha serikali ya mpito ya wanaume pekee ikiita Imarati ya Kiislam ya Afghanista (Islamic Emirate of Afghanistan).

Kundi hilo lenye msimamo mkali liliwaruhusu wanafunzi wa kike wa chuo kikuu kurejea chuoni katika mfumo mpya ulioelezewa wa elimu unaotenganisha jinsia. Lakini licha ya kuahidi mara kwa mara kuwaruhusu wasichana wa Afghanistan kurudi kwenye madarasa yao Taliban bado hawajafungua tena shule za sekondari kwa wasichana.

XS
SM
MD
LG