Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:57

Rais wa Guinea Bissau amevunja bunge na anadai ataitishwa uchaguzi wa mapema


Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló akiongea na vyombo vya habari katika picha iliyochukuliwa Februari Mosi, 2022
Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embaló akiongea na vyombo vya habari katika picha iliyochukuliwa Februari Mosi, 2022

Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo siku ya Jumatatu alivunja bunge la nchi hiyo na kusema kuwa utaitishwa uchaguzi wa mapema mwaka huu ili kutatua mzozo wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu.

Mvutano kati ya bunge na urais umelikumba taifa hilo la Afrika magharibi kwa miezi kadhaa. Embalo alitaja tofauti zinazoendelea na zi-sizoweza kutatuliwa na bunge, ambazo alielezea nafasi ya siasa za msituni na njama.

Mgogoro huu wa kisiasa umemaliza mtaji wa uaminifu kati ya taasisi huru, alisema. “Nimeamua kurudisha nafasi kwa wa-Guinea ili mwaka huu waweze kuchagua kwa uhuru bunge wanalotaka kuwa nalo”. Amri ya Rais ilisema uchaguzi wa bunge utafanyika Disemba 18.

XS
SM
MD
LG