Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:14

Marekani iko tayari kuyaondoa makundi yenye msimamo mkali yanayoaminika kuacha harakati hizo


Wizara Ya Mambo Ya Nje Marekani
Wizara Ya Mambo Ya Nje Marekani

Marekani iko tayari kuyaondoa makundi matano yenye msimamo mkali ambayo yote yanaaminika kuwa hayafanyi harakati zao na kutolewa katika orodha yake ya taasisi za kigaidi za kigeni yakijumuisha makundi yaliyowahi kutoa tishio kubwa na kuua mamia kama sio maelfu ya watu kote Asia, Ulaya na mashariki ya kati.

Ingawa vikundi hivyo havifanyi kazi uamuzi huo ni nyeti wa kisiasa kwa utawala wa Biden pamoja na nchi ambapo mashirika hayo yalifanya kazi na yanaweza kukosolewa na waathirika pamoja na familia zao ambazo bado zinakabiliana na machungu ya kupoteza wapendwa wao.

Mashirika hayo ni pamoja na kundi linalotaka kujitenga la Basque ETA, dhehebu la kijapani la Aum Shinrikyo, kundi la kiyahudi lenye itikadi kali Kahane Kach, na makundi mawili ya kiislam ambayo yamekuwa yakifanya harakati zao huko Israel, mamlaka ya wapalestina na nchini Misri.

Wizara ya mambo ya nje Marekani ililiarifu bunge siku ya Ijumaa kuhusu hatua hizo ambazo zinakuja wakati kuna mjadala unaozidi kuleta mgawanyiko lakini hauhusiani na Washington na kwingineko kuhusu iwapo jeshi la walinzi wa mapinduzi ya kijeshi la Iran linafaa au linaweza kuondolewa kisheria katika orodha ya Marekani kama sehemu za kuokoa mapatano ya nyuklia ya Iran yanayodorora.

XS
SM
MD
LG