Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 17:45

Marekani inapanga kuelezea sera yake kwa China kabla ya mkutano wa June


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Marekani inapanga kuelezea kikamilifu sera yake kwa China kabla ya mfululizo wa mikutano ya ngazi ya juu na viongozi wa Asia na mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya wakuu wa ulinzi wa Marekani na China hapo mwezi June.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken alitarajiwa kutoa hotuba muhimu wiki hii kuelezea mtazamo wa utawala kwa uhusiano wake na China. Hotuba hiyo iliahirishwa baada ya waziri huyo siku ya Jumatano kugundulika kwamba amepata maambukizi ya COVID-19.

Sera ya Marekani kwa China huwenda ikawa sehemu ya mkutano wa viongozi wa Marekani na ASEAN wiki ijayo mjini Washington pamoja na mkutano wa Quad baadae mwezi huu mjini Tokyo ambapo Rais Joe Biden atakutana na viongozi wenzake kutoka Australia, India na Japan.

Rais Biden amesisitiza kwamba Washington na Beijing zinahitaji kupanua ulinzi ili kuepusha migogoro isiyotarajiwa wakati wakikabiliana na ushindani mkubwa wa mamlaka na China.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG