Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:26

Marekani imefungua tena ubalozi wake nchini Cuba


Jengo la ubalozi wa Marekani nchini Cuba
Jengo la ubalozi wa Marekani nchini Cuba

Ubalozi wa Marekani nchini Cuba ulianza kutoa visa siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza tangu madai ya mashambulizi ya mfumo wa sauti (Sonic Attacks) dhidi ya wafanyakazi wa kidiplomasia zaidi ya miaka mine iliyopita.

Washington ilifunga huduma zake za kibalozi katika mji mkuu wa Cuba mwaka 2017 baada ya wafanyakazi wa marekani na familia zao kuugua magonjwa ya ajabu yaliyojulikana kama Havana Syndrome. Kufungwa huko kulikuwa pigo kubwa kwa wa-Cuba wengi wanaotarajia kuhamia Marekani na kuepuka matatizo ya kiuchumi ya taifa hilo.

Karibu katika ubalozi baada ya muda mrefu, mfanyakazi wa Cuba alisema kwa kundi dogo la watu waliokuwa wanasubiri fursa kupewa nafasi ya kuingia kwenye ubalozi huo mdogo.

Marekani ilitangaza miezi miwili iliyopita itaanza kufungua tena kidogo na taratibu, kwa ubalozi wake na huduma za kibalozi. Ulifungwa Septemba mwaka 2017 baada ya Rais wa wakati huo Donald Trump kuelezea madai ya shambulizi hilo la Sonic.

XS
SM
MD
LG