Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 05:36

Maambukizi mapya ya COVID Marekani yanaibua kundi jipya hatarishi


Mfano wa virusi vya COVID-19
Mfano wa virusi vya COVID-19

Kuongezeka kwa maambukizi ya COVID-19 kote Marekani kumepelekea miji mingi kuingia kwenye kundi jipya hatarishi ambalo linapelekea kuchochea uvaaji wa barakoa ndani ya majengo lakini sehemu kubwa ya nchi imeacha kurudisha masharti ya kukabiliana na COVID huku kukiwa na ongezeko kwa kiasi Fulani.

Kwa wiki kadhaa sehemu kubwa ya jimbo la New York imekuwa katika kiwango cha juu cha onyo chenye rangi ya machungwa, kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa (CDC) ambapo kinaelezea kasi ya kuenea kwa maambukizi.

CDC inawasihi watu kuvaa barakoa katika maeneo ya ndani ya umma, ikiwemo shule bila kujali hali yako kama umechoma chanjo au la. Lakini wachache ikiwemo mamlaka za eneo kwenye mkoa huo zilirudisha umuhimu wa kuvaa barakoa kufuatia kuongezeka kwa kesi.

Katika jiji la New York kesi zinaongezeka tena na wiki hii zilivuka kiwango cha jiji cha “hatari ya wastani” ikionyesha kuenea kwa kasi kwa aina ya kirusi kijulikanacho BA-2 ambacho kimeenea maeneo ya kaskazini mwa jimbo hilo.

XS
SM
MD
LG