Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatatu aliisihi jumuiya ya kimataifa kuwekeza kikamilifu kuisaidia Niger, nchi maskini sana kupambana na waasi wa Jihadi wanaoitishia serikali huko Niamey na nchi jirani.
Leo ninaamini kwa kuangalia utendaji wa kipekee wa jeshi la Niger jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwekeza kikamilifu ili kuimarisha uwezo wa jeshi la Niger alisema Guterres akiwa pamoja na Rais wa taifa hilo la Sahel Mohamed Bazoum.
Vifaa na mafunzo vinahitajika Guterres alisema. Niger haiwezi kukabiliana na changamoto hizi nyingi peke yake aliongeza akiorodhesha mashirika makubwa kama vile Umoja wa Afrika, Jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS) ambao ni wahusika wakuu wa amani na maendeleo katika eneo hilo.
Guterres alikiri hata hivyo kwamba G5-Sahel ambayo inawajumuisha Mauritania, Mali, Burkina faso, Niger na Chad imedhoofishwa na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea katika baadhi ya majirani zao akimaanisha Mali na Burkina Faso katika muda wa kipindi cha miaka miwili iliyopita.