Mamlaka ya magereza nchini Morocco imekuwa ikitoa mafunzo ya kutokomeza ugaidi tangu mwaka 2017 kwa wapiganaji wa zamani wa kundi la Islamic State (IS) na wengine waliopatikana na hatia ya makosa ya ugaidi.
Program ya tisa ya kundi la wahitimu lilimaliza masomo wiki iliyopita. Shirika la habari la Associated Press na vyombo vingine vya habari walialikwa kushuhudia sherehe zao za kuhitimu katika gereza la Sale karibu na mji mkuu Rabat.
Kuhitimu kutoka kwenye mpango huo hakufanyi wafungwa wastahiki moja kwa moja kuachiliwa mapema lakini kunaongeza fursa zao za kupata msamaha au kupunguziwa adhabu. Mhitimu mmoja alisema ameona maovu yote ya vita kama mpiganaji wa kundi la Islamic State na akagundua kwamba vita havikuwa na uhusiano wowote na dini zetu. Anasema sasa amekanusha itikadi kali.