Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:20

Makundi yenye silaha huko Chad yashutumu kuyumba kwa mazungumzo ya amani ya Qatar


Washiriki katika mazungumzo ya kuleta amani nchini Chad yanayofanyika Doha, Qatar
Washiriki katika mazungumzo ya kuleta amani nchini Chad yanayofanyika Doha, Qatar

Makundi ya waasi wenye silaha nchini Chad siku ya Alhamis yaliushutumu mji wa Njamena kuzorotesha kwa makusudi mazungumzo huko Qatar ambayo yamebuniwa ili kuandaa mazungumzo ya kitaifa na uchaguzi baadae mwaka huu.

Taifa hilo la Afrika lisilo na bandari lilikumbwa na misukosuko baada ya kiongozi wa muda mrefu Idriss Deby Itno kufariki akipambana na waasi hapo April mwaka jana. Mtoto wake wa kiume, Mahamat Idriss Deby Itno alinyakua udhibiti lakini ameahidi kufanyika uchaguzi huru mwaka huu.

Mazungumzo ya maandalizi ya Doha yalianza Machi 13 baada ya kuchelewa kwa wiki mbili na yaliandaliwa kabla ya mazungumzo ya kitaifa hapo Mei 10 yakifuatiwa na katiba mpya na uchaguzi utakaofanyika ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Maelfu ya makundi yenye silaha na wanaharakati wa kisiasa wasio na silaha wanahusika katika mchakato wa Qatar lakini wote wanaripotiwa kukataa kuzungumza moja kwa moja na serikali.

Baada ya kuvuruga kwa makusudi mazungumzo hayo kwa kukosekana mara kwa mara kwa wawakilishi waandamizi, serikali inajaribu kuharakisha na kusitisha upinzani wa kisiasa na kijeshi kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa, makundi hayo yalisema katika taarifa.

XS
SM
MD
LG