Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 03:02

Miaka minane tangu utekaji nyara wa wasichana wa Chibok huko Nigeria


Wanaharakati wa Bring Back Our Girls katika juhudi za kupatikana wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram. Lagos, Nigeria, April. 13, 2017.

April 14 imetimia miaka 8 tangu kundi la kigaidi la Boko Haram lilipofanya shambulizi mwaka 2014 kwenye shule ya sekondari ya wasichana huko Chibok katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwateka nyara wasichana 276 waliokuwa wakifanya mitihani yao ya kumaliza shule.

Tukio hilo limepelekea wasichana wengi na wanafunzi kutekwa nyara wakiwa shuleni au majumbani mwao na hata barabarani wakati wanaposafiri. Magaidi wamekuwa wakidai mamilioni ya dola kama fidia kutoka kwa familia na wazazi wa waathirika wao.

Utekaji nyara wa wasichana hao kutoka Chibok bado haujapatiwa ufumbuzi hadi wakati huu. Hii ni kwasababu wasichana wapatao 110 kati ya jumla ya wale waliotekwa bado hawajapatikana licha ya juhudi za kuwatafuta zinazofanyika.

Mmoja wa wanaharakati wa kikundi la Bring Back Our Girls, Aisha Yesufu anasema ni muhimu kwa serekali kufanya mikakati thabiti ya kuwaokoa wasichana hao kutoka kwa magaidi bila kuchelewa tena.

Mwanaharakati wa haki za wanawake Bridget Osakwe Osifo na Mwanaharakati wa haki za binadamu Emmanuel Ogebe wanasema kuwa serikali kushindwa kuwaokoa wasichana hao waliosalia licha ya ahadi kadhaa kuwa watawapata kunawapa wasi wasi iwapo wasichana hao wataweza kweli kutoka kwenye mikono ya magaidi.

Makamu Spika wa baraza la wawakilishi Idris Wase anasema mwanajeshi mmoja alikamatawa katika wilaya yake akitoa nguo za kijeshi kwa magaidi ili wazitumie na pia Jumanne iliyopita askari mmoja alikamatwa na jeshi la usalama akijaribu kupeleka takribani dola elfu 116 kwa magaidi ikiwa ni sehemu ya fidia kutoka kwa familia ya waathirika. Alifanya hivyo kwa siri.

Jumatano magaidi walishambulia shule ya afya katika jimbo la Zamfara na kuwateka wasichana 5. Hii ni licha ya wathirika 146 waliopo katika mikono ya magaidi kufuatia tukio la shambulizi la treni ya Abuja kwenda Kaduna karibu wiki tatu zilizopita.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG