Polisi wa Morocco wamewakamata watu wane wanaoshukiwa kuhusika na mtandao wa kimataifa wa ulanguzi wa dawa za kulevya na viungo vya binadamu unaofanya kazi kati ya Morocco na Uturuki chanzo cha usalama kilisema Jumanne.
Mamlaka ilianzisha uchunguzi baada ya tangazo lililochapishwa kwenye mitandao ya kijamii likipendekeza kuondolewa kwa figo katika kliniki moja ya binafsi nje ya nchi kwa malipo ya pesa nyingi za kigeni kitengo cha usalama cha DGSN kilisema katika taarifa.
Washukiwa hao wane wakiwemo wanawake watatu wanadaiwa kuwa watu wa kati wakiwasaidia wale wanaotaka kuuza viungo vyao vya ndani vya mwili kwenda nje ya nchi hasa uturuki. Waathirika wawili wametambuliwa huku wengine wakidaiwa kulazimishwa kupokea pamoja na kusafirisha dawa za kulevya nchini Morocco na kwingineko taarifa hiyo iliongeza.
Shughuli hizo zilifanywa kwa kushirikiana na mtandao wa kihalifu unaoendesha operesheni zake nje ya Morocco unaoundwa na raia wa kigeni waliohusika katika kuondolewa watu na uuzaji wa viungo vya ndani vya binadamu DGSN ilisema.