Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:39

Rais Biden ametangaza mipango ya kupanua bima ya afya ya bei nafuu


Rais Joe Biden akitangaza mpango wa kupanua fursa katika huduma ya afya ya bei nafuu. April 5, 2022
Rais Joe Biden akitangaza mpango wa kupanua fursa katika huduma ya afya ya bei nafuu. April 5, 2022

Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza mipango ya kupanua fursa za huduma za afya kwa kupendekeza mabadiliko ya sheria ya huduma ya afya ya bei nafuu (ACA) ili kuruhusu mamilioni ya familia za Marekani kununua mipango ya bima ya afya na kupata ahueni ya kodi ili kupunguza gharama.

Wakati kanuni inayopendekezwa leo itakapokamilika, kuanzia mwaka ujao, familia zinazofanya kazi zitapata msaada wanaohitaji kumudu huduma kamili ya bima ya familia kwa Kila mtu katika familia, Biden alisema katika hotuba yake huko White House kabla ya kutia saini amri ya kiutendaji kuboresha fursa ya Affordable Care Act and Medicaid”.

Biden aliandamana na Makamu Rais kamala Harris na rais wa zamani Marekani, barack Obama ambaye Machi 10 mwaka 2010 alitia saini ACA, sheria ya afya inayojulikana kama ObamaCare.

Hii ni ziara ya kwanza ya Obama kurejea White House tangu alipoondoka madarakani mwaka 2017 baada ya kuhudumu mihula miwili akiwa na Biden wakati huo kama Makamu Rais wake.

XS
SM
MD
LG